Karibu
Chama Cha Sarufi ya Kiswahili Tanzania kwa Sarufi. Uchambuzi. Semina. Mafunzo. Makala.
CHASAKITA ni chama kilichoanzishwa kwa lengo la kukuza, kulinda na kuendeleza Sarufi ya Kiswahili nchini Tanzania na nje ya nchi. Kuanzishwa kwake kulitokana na changamoto za Sarufi ya Kiswahili kuonekana kuwa ngumu kwa wanafunzi na walimu pamoja na kutokuwa na nafasi kubwa katika soko la ajira. Chama hiki kinalenga kusimamia maendeleo ya Sarufi ya Kiswahili katika sera, mitaala na ufundishaji ili kuimarisha matumizi na hadhi yake.
Makala yote
MAJUKUMU YA CHASAKITA
Kuikuza na kuieneza sarufi ya Kiswahili
Kwa kushiriki mihadhara semina na makongamano
Kuendesha shughuli za kitaaluma,
kijamii na kitamaduni kuhusu Sarufi na Isimu ya Kiswahili.
Kujenga uhusiano na kushirikiano
Hasa na asasi nyingine za kitaifa, kikanda na kimataifa zinazounga mkono uendelezaji wa Kiswahili.
Kuhimiza ufundishaji na usomaji wa taaluma mbalimbali,
Kama tafsiri na ukalimani, pamoja na kuimarisha shughuli hizo
Kutoa mafunzo ya muda mfupi
Ili kuongeza uchechemuzi wa kisarufi kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili.
Kutoa mafunzo ya kufundisha Kiswahili kwa wageni.
Mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi
Ujumbe wa Mwenyekiti
Mahenda Kulwa Jagadi -Mwenyekiti na Muasisi -CHASAKITA
Ndugu wanachama, wadau wa lugha ya Kiswahili, walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla, Napenda kukukaribisheni katika Chama cha Sarufi ya Kiswahili Tanzania (CHASAKITA), taasisi iliyoanzishwa kwa dhamira ya kuenzi, kulinda na kuendeleza Sarufi ya lugha ya Kiswahili sanifu nchini Tanzania na nje ya mipaka yake. CHASAKITA imeanzishwa kutokana uhitaji mkubwa wa kuwa na chombo maalumu kitakachofuatilia kwa karibu maendeleo ya Sarufi ya Kiswahili kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi elimu ya juu, pamoja na matumizi yake katika jamii na taasisi mbalimbali. Kwa muda mrefu, Sarufi ya Kiswahili imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo kuonekana kuwa ni ngumu kwa wanafunzi na baadhi ya walimu, kudunishwa hadhi yake, pamoja na .... ... mtazamo hasi kuwa haina nafasi pana katika soko la ajira huria. Hali hii imekuwa changamoto kubwa katika ukuaji na ustawi wa lugha hii. Kutokana na hali hiyo, wanachama na wadau wa Sarufi ya Kiswahili waliona umuhimu wa kuungana na kuanzisha chama hiki ili kiwe dira ya kuratibu, kuhamasisha na kuimarisha juhudi za kukuza Sarufi ya Kiswahili kwa kuzingatia misingi ya taaluma, sheria za nchi na mahitaji ya jamii ya sasa ijayo. CHASAKITA inalenga kuimarisha ufundishaji na ujifundishaji wa Sarufi ya Kiswahili, kuendeleza tafiti mbalimbali zinazohusu lugha ya Kiswahili, kusambaza matokeo ya tafiti hizo, pamoja na kuhakikisha kuwa Sarufi ya Kiswahili inapewa nafasi na hadhi inayostahili katika sera, mitaala ya elimu na matumizi ya kila siku ndani na nje ya Tanzania. Matarajio yetu makubwa ni kuona walimu wa Sarufi ya Kiswahili, wanafunzi na jamii kwa ujumla wanapata elimu sahihi kuhusu umuhimu wa kuenzi, kutunza na kuendeleza Sarufi ya Kiswahili. Tunaamini kuwa kupitia elimu, uhamasishaji na ushirikiano wa pamoja, tutaweza kujenga jamii yenye mtazamo chanya kuhusu Sarufi ya Kiswahili. Kwa niaba ya uongozi wa CHASAKITA, ninawaalika wadau wote kushirikiana nasi katika safari hii muhimu ya kuikuza na kuiendeleza Sarufi ya Kiswahili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Karibuni sana Mahenda Kulwa Jagadi Mwenyekiti na Muasisi Chama cha Sarufi ya Kiswahili Tanzania (CHASAKITA)
Chama Cha Sarufi ya Kiswahili Tanzania-CHASAKITA
Matarajio makuu ya CHASAKITA ni kuhakikisha kuwa walimu wa sarufi ya Kiswahili na jamii wanapata elimu ya kutosha kuhusiana na mambo muhimu katika kuenzi, kutunza na kuendeleza sarufi ya lugha ya Kiswahili ili kusaidia uwepo wa jamii ambayo itakuwa na mabadiliko na mitazamo mipya na hatimaye kutokuwa na jamii iliyo na mitazamo hasi juu ya sarufi ya lugha na kufanikisha uwepo wa jamii itakayoenzi, kutunza na kuendeleza sarufi ya lugha ya Kiswahili na tunatarajia kuwa, jamii itaweza kujivunia sarufi ya lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania..
Ungana nasiMatarajio
kuhakikisha kuwa walimu wa sarufi ya Kiswahili na jamii wanapata elimu ya kutosha kuhusiana na mambo muhimu katika kuenzi, kutunza na kuendeleza sarufi ya lugha ya Kiswahili
Malengo
Kuimarisha misingi ya sarufi ya Kiswahili kwa walimu wa Kiswahili nchini ili kuongeza uelewa na ari ya kutaka kuienzi, kuitunza na kuieneza sarufi ya Kiswahili
Msingi
kukuza na kuendeleza sarufi ya Kiswahili sanifu kitaifa na kimataifa kupitia mafunzo ya kitaaluma, warsha, uandishi na uchapishaji.
Taarifa Mpya
Shughuli za mawanda
Semina
Warsha
Wanachama
Wanachama wapya
Viongozi Waandamizi
Maendeleo ya CHASAKITA yanachagizwa na wanachama pamoja na viongozi mahiri.
Mwenyekiti
M/kiti-Kamati tendaji
Katibu
Mhazini